UWT waanza ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha sabuni mkoani Njombe | Tarimo Blog

 Na Amiri Kilagalila,Njombe

Jumuiya ya umoja wa wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Njombe,imezindua na kuanza ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha sabuni mbali mbali katika kata ya mji Mwema halmashauri ya mji wa Njombe ili kuendelea kukuza na kuongeza vyanzo vya mapato vya jumuiya hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua zoezi la ujenzi huo mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Njombe Jassel Mwamwala amesema jumuhiya hiyo inazidi kuonyesha njia katika kutafuta vyanzo vya mapato na kufungua fursa za ajila hivyo anaamini kiwanda hicho kitakuwa na manufaa makubwa kwa taifa.

“Hii ni njia ya kufanya jumuiya hii izidi kujitegemea kwa ajili ya uchumi wetu na kwa taifa na leo mkoa wa Njombe wakina mama mnakwenda kutuondoa kwenye omba omba niwapongeze sana”alisema Mwamwala

Aidha ameitaka Jumuiya hiyo kujipanga zaidi ili kukamilisha kiwanda hicho kitakacho leta faida kwa kuwa sabuni zimekuwa zikitumika kwa kiasi kikubwa.

“Sabuni nyingi tunazipata kutoka Dar es Salaam na mikoa mingine sasa leo tunaambiwa sabuni zitatoka Njombe kwa hili hongereni sana lakini jambo jingine mmenifurahisha kuwa malighafi mojawapo itayotumika ni parachichi na sisi tunazalisha parachichi hili ni jambo zuri sana”aliongeza Mwamwala

Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Scolastika Kevela amesema ujenzi wa kiwan


Mwenyekiti wa Chama cha Mapnduzi mkoa wa Njombe Jassel Mwamwala pamoja na mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Scolastika Kevela wakishiriki zoezi la ujenzi ili kuonyesha umoja na uzinduzi rasmi wa ujezni wa Kiwanda hicho.



Mwenyekiti wa Chama cha Mapnduzi mkoa wa Njombe Jassel Mwamwala akizungumza na wanawake katika eneo la ujenzi wa kiwanda mara baada ya uzinduzi wa ujenzi wa jengo la kiwanda




da hichi ni moja ya mipango mikubwa ya jumuiya katika kujikomboa kiuchumi na wanatarajia kuzalisha sabuni za aina mbali mbali ikiwemo sabauni ya maji,ya kuogea pamoja na za kufulia.

“Tutazalisha sabuni za kuogea,za kufulia,vitakasa mikono na nyingine nyingi na mradi huu utakapo kamilika utaleta ajira pamoja na kuwasaidia wakulima wa parachichi kwa kuwa hapa itakuwa ni soko,na pia hatutategemea soko letu kuwa Njombe tu tutaenda mpaka nje ya nchi”alisema Scolastika Kevela

Rehema Nyenzi na Sina Mtandika ni baadhi ya wanawake wa jumuiya hiyo wamesema wanaamini ujenzi wa kiwanda hicho na kukamilika utakuwa manufaa makubwa kwao ikiwemo kupata sabuni kwa haraka na kupeleka katika vibanda vyao.

“Tumezoea kufanya biashara zingine ndogo ndogo ninaimani kuwa tutakuwa na uwezo wa kuchukua sabauni hapa na kupeleka kwenye vibanda vyetu huko mjini”alisema Rehema Nyenzi

Sina Mtandika amesema “Wakina mama tunajua sabuni muhimu sana na huwezi ukakaa siku mbili bila kuitumia kwa maana hiyo hatuna budi kushukuru kujengwa kwa kiwanda hiki”

Kwa mujibu wa taarifa ya mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe amesema mpaka kiwanda hicho kukamilika kinatarajiwa kujengwa kwa ghalama ya zaidi ya milioni mia mbili arobaini na tano huku kikiwa na uwezo wa kuzalisha sabuni zaidi ya katoni mia mbili kwa siku.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2