WATU WATATU WADAIWA KUWAWA KIKATILI MKOANI PWANI. | Tarimo Blog

 Na Scolastica Msewa, Kibaha.


Watu watatu wameuawa katika matukio matatu tofauti likiwemo la kuuawa kwa kukatwa shingo kisha kutenganisha kichwa na kiwiliwili huko Bagamoyo mkoani Pwani na mkulima mmoja ameuawa kwa kupigwa mkuki na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafugaji .

Akizungumza na Waandishi wa habari mjini kibaha Kamanda wa polisi mkoa Pwani ACP Wankyo Nyigesa amesema matukio hayo ni matokeo ya oparasheni iliyofanyika kati ya tarehe 31 july mwaka huu hadi August 9 mwaka huu.

Alisema Mnamo tarehe 4/8/2021 majira ya saa 12:00 huko kijiji cha Kitonga, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani (Ke), Miaka 70, Mndengereko, mkazi wa kitonga aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali shingoni kisha kutenganisha kichwa na kiwiliwili.

Msako mkali unaendelea ili kuwakamata waliohusika na tukio hilo.

Wakati huo huo mnamo tarehe 8/8/2021 majira ya saa 9:00 huko kitongoji cha Tobora kata ya Msata, Wilaya ya Kipolisi Chalinze Mkoa wa PWANI, (ke), Miaka 26, Mzigua, Mkulima, Mkazi wa Pongwe Msungura alibakwa kisha kuuawa ambapo Mtuhumiwa mmoja amekamatwa kuhusiana na tukio hili.

Katika tukio jingine, huko Chalinze kwa ng'wandu Mbwewe jina limehifadhiwa mtu mmoja aliuawa saa 6 mchana akiwa katika ukaguzi wa shughuli za shamba watu wasiojulikana walimchoma mkuki na watu wanaosadikiwa kuwa ni jamii ya wafugaji na kusababisha kifo chake.

Wankyo alisema wanaendelea na uchunguzi ilikuwapata watuhumiwa wa tukio hilo.

Hatahivyo Kamanda Wankyo akizungumzia kupatikana na sare za jeshi la Polisi alisema mnamo tarehe 5/8/2021 majira ya saa 5:30 Usiku, huko maeneo ya Kibondeni, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani alikamatwa Otto William@ chacha, Miaka 28, Mjaruo, Mkulima Mkazi wa Kibondeni akiwa na Sare za Jeshi la Polisi ambazo ni, General Duty (Khaki) pea 3, Mkanda wa bendera 1, mkanda wa JKT 1, Ballet 1, buti pea 3, mbili nyeusi na moja ya khaki, begi dogo la mgongoni na sweta. Mtuhumiwa amekematwa kwa hatua zaidi.

Aidha kuhusu kupatikana na silaha Kamanda Wankyo alisema mnamo tarehe 4/8/2021 majira ya saa 11:00 jioni huko Msimbani, Kata ya Miono, Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani  alikamatwa Sijali Iddi akiwa na Gobole 1,unga wa baruti na goroli 11 za zinazotumika katia gobole hilo. baada ya upelelezi kukamilika mtuhumiwa amefikishwa mahakamani.







 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2