Na John Walter-Babati
Chama Cha Mapinduzi kimefurahishwa na kupongeza zoezi la ujenzi wa vyumba vya madarasa 18 ya shule za sekondari ndani ya Jimbo la Babati Mjini kutokana na fedha za mpango wa maendeleo dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19 kiasi cha shilingi Bilioni 1,087,500,000 zilizotolewa na Rais Mhe Samia Suluhu Hassan.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Babati Mjini Mheshimiwa Elizabeth Marley wakati wa makabidhiano ya madarasa 18, zoezi lililofanyika katika shule ya sekondari Komoto ambapo amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kutoa fedha hizo zitakazosaidia kupunguza kero ya michango Kwa Wazazi na changamoto ya watoto kubanana kwa ufinyu wa vyumba vya madarasa.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Babati Lazaro Twange akipokea madarasa hayo ameridhishwa na ubora uliokidhi viwango vilivyohitajika na kuwaasa wananchi kuendelea kushirikiana na Serikali pamoja na kumshukuru Rais Samia Kwa kuendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi mbalimbali ya maendeleo katika wilaya hiyo.
Twange amesema Ujenzi huo wa madarasa kwa fedha za Rais zimepunguza kwa kiwango kikubwa changamoto ya uhaba wa madarasa ambayo ilikuwa kwa muda mrefu hali iliyokuwa inawalazimu wananfunzi kusongamana darasani.
Halmashauri ya mji wa Babati imekuwa ya kwanza katika mkoa wa Manyara kukamilisha na kukabidhi vyumba vya madarasa kwa Mkuu wa mkoa wa wilaya Lazaro Twange kwa ajili ya maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato Cha kwanza mwakani 2022.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Babati Faustine Masunga akisoma taarifa ya mradi huo amesema kupitia mradi namba 5441-TCRP hadi sasa wamepokea kiasi cha shilingi 778,515,988.08 ambapo Shilingi 28,515,998 ni kwa ajili ya uhamasishaji wa chanjo na 750,000,000 kwa ajili ya miradi ya miundo mbinu katika sekta ya Elimu na Afya.
Masunga amesema katika fedha hizo shilingi 360,000,000 ni kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 18 Sekondari na msingi huku shilingi Milioni 300,000,000 zikiwa ni kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura katika hospitali ya mji wa Babati (MRARA), shilingi 90,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi 3 kwa 1 kituo cha afya Mutuka.
Aidha kwa upande wa ujenzi wa Madarasa hayo 18 ambao umegharimu shilingi 379,267,500 zikiwemo za mradi 360,000,000 wa Uviko 19, shilingi 19,267,500 ni nguvu za wananchi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment