RAIS SAMIA:WANAODHANI KUNA KUSIMAMISHWA UJENZI WA MIRADI ILI WAPATE KUSEMA HILO HALIPO | Tarimo Blog




*Asema Serikali itaendelea kukopa kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maaendeleo

Na Said Mwishehe, Michuzi Blog

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameweka wazi kwamba kama wapo waliodhani kuna kusimamishwa ujenzi wa miradi ili wapate la kusema hilo halipo, na wataendelea na ujenzi,hakuna utakaosimama.

Amesema hayo leo Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kushuhudia utiwaji saini wa makubaliano ya mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha tatu kutoka Makutupora hadi mkoani Tabora chenye urefu wa kilomita 368.

"Tutendelea na ujenzi wa miradi,kuna jitihada za kutuvunja moyo katika mikopo hakuna nchi isiyokopa hata hizo zilizoendelea wanamikopo mikubwa kuliko ya kwetu,tutakopa tumalize miradi ya maaendeleo kwasababu ukikopa unajengaa sasa kwa haraka, kuharakisha maendeleo,ukisubiri ukusanye za kwako utamaliza lini kujenga? Mradi wa matrilioni ,mradi wa matrilioni unasibiri ukusanye za kwako unamaliza lini?Lakini kopa,kusanya,nenda kalipe polepole, na wakopaji wanakupa muda mpaka miaka 20."

Akielezea zaidi mradi wa ujenzi huo wa reli amesema utakagharimu Shilingi trilioni 4.41 na umesainiwa kati Serikali kupitia Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Yapi Merkez kutoka nchini Uturuki huku akifafanua mradi wa SGR ulianza kutekelezwa kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"Awamu ya kwanza ya ujenzi ni kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza ambao ulianza 2017 na umegawanyika katika vipande vitano ukipita katika mikoa tisa.Uujenzi huo unaendelea katika vipande vitatu cha Dar es Salaam- Morogoro asilimia 95, Morogoro- Makutupora asilimia 77 na Mwanza-Isaka asilimia nne, ambapo ni jumla ya kilomita 1,063 za njia kuu za reli pamoja na njia za kupishana,"amesema Rais Samia na kuongeza hiyo ni kazi kubwa yenye kuhitaji uthubutu mkubwa wa Serikali na wananchi wake.

Amesisitiza kuwa hiyo inafanya uwekezaji wa ujenzi wa vipande vinne kati ya vitano vinavyoendelea kufikia kiasi cha Sh trilioni 14.7 ukijumlisha na kodi."Niwaahidi tutaendeleza mema yaliyopita, yaliyopo na kuanzisha mema mapya, ujenzi na utekelezaji wa miradi yote iliyoanzishwa na inayoendelea Serikali itaendelea kuisimamia na kuhakikisha inakamilika kwa wakati".

Ametumia nafasi hiyo kueleza hakuna mkandarasi anayedai hata sent ila Serikali ndio inayodai ukamilishwaji wa miradi, lakini kuna watu ambao walipenda kuona miradi hii haiendelezwi na wanathubutu kusema miradi hiyo imeshindikana, haiendelezwi.

Aidha amegusia ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Mwalimu Nyerere ambalo utekelezaji wa ujenzi unakwenda vizuri na wala hakuna deni.

Katika hatua nyingine,Rais Samia amesema tayari wamengia mkataba wa ununuzi wa mabehewa ya abiria 89, vichwa vya treni ya umeme 19, seti za treni za kisasa 10 zenye mabehewa 80 vikiwa na gharama ya dola za Marekani milioni 381.43 na serikali inaendelea kukamilisha ununuzi wa mabehewa ya mizigo 1430 yen ye thamani dola za Marekani milioni 127.21.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2