JESHI la Polisi mkoa wa Morogoro limeendelea kuimarisha doria na misako na kufanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 44 wa makosa mbalimbali pamoja na gari 01 ikisafirisha matapeli wa wizi kwa njia ya mitandao, Mirungi bunda 49, Pikipiki 01 ikisafirisha mirungi hiyo, mapanga 04 na visu 04.
Mnamo tarehe 30/07/2020 ilipokelewa taarifa katika kituo cha Polisi Dumila ya mwanamke mmoja kutapeli kwa njia ya mtandao na baada ya ufuatiliaji kupitia kitengo maalum cha makosa ya wizi kwa njia ya mitandao (Cyber Crime) Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro limefanikiwa kuwatia mbaroni jumla ya watuhumiwa sugu 05 wa makosa ya wizi kwa njia wa mitandao ambao wamewahi kufanya matukio hayo ya wizi katika mikoa ya Rukwa (Sumbawanga), Arusha, Dodoma, Mbeya, Dar es salaam, Shinyanga, Mwanza na Kilimanjaro (Moshi).
Watuhumiwa hao ni: ZUHURA D/O ALLY, Miaka 33, mkazi wa Mwanza, HERI S/O IBRAHIM, Miaka 30, mkazi wa Mwanza, YASIN S/O JUMA, Miaka 30, Mkazi wa Mwanza, ISAYA S/O ERASTO, Miaka 32, Mkazi wa Arusha, GOODLUCK S/O RICHARD, Miaka 32, Mkazi wa Arusha.
Awali siku yatarehe 30/07/2020 majiraya saa 05 asubuhi hukoma eneo ya kijiji cha Dumila juu, kata ya Dumila, wilaya ya Kilosa, mkoa wa Morogoro PENDO D/O AMOS, Miaka 29, Mfanya biashara, Mkazi wa Dumila alitaka kuibiwa kiasi cha Tshs 300,000/= kwanjia ya mtandao na ZUHURA D/O ALLY, Miaka 33, mkazi wa Mwanza mwenye namba ya simu 0714545649 baada ya kupokea ujumbe wa kutoa fedha kwa wakala wa fedha kwa kutumia meseji ya uongo kuonyesha kuwa kimetolewa kiasi cha Tshs 300,000.
Mlalamikaji alipogundua kuwa anataka kuibiwa aliwahi kutoa taarifa kituo cha Polisi na baada ya ufuatiliaji kupitia kitengo maalum cha makosa ya wizi kwa njia ya mitandao cha Jeshi la Polisi alikamatwa na wenzake 04 wakiwa safarini kuelekea Mwanza wakitumia gari yao aina ya Toyota Carina yenye namba T.620 BYM ambayo huwa wanaitumia katika shughuri zao za utapeli.
Watuhumi wa wamehojiwa na kukiri kufanya matukio hayo ya utapeli na wizi katika mikoa mbalimbali nchini na mara upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani.
Hata hivyo Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro Mnamo tarehe 11/08/2020 majira ya saa 08 usiku huko maeneo ya kijiji cha Minjeja kilichopo katika kata ya Ukwamani tarafa na wilaya ya Gairo mkoa wa Morogoro askari Polisi wakiwa doria na misako ghafla walimuona mtu na kumtilia mashaka walipomfuata alikimbia na kutelekeza pikipiki aina ya Haojue nyenye namba MC 239 BBH ikiwa na kiroba 01 na baada ya askari kukagua kiroba na pikipiki hiyo walibaini kimehifadhiwa dawa za kulevya aina ya Mirungi bunda 49 zenye uzito wa Kg 22 na pikipiki hiyo inahisiwa kuwa ni mali ya wizi kwani haina chases na engine namba.
Mtuhumiwa anaendelea kutafutwa na akikamatwa atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yake.
Hata hivyo Mnamo tarehe 8/8/2020 majira ya saa 10 jioni na kuendelea, Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro liliendelea kuimarisha doria na misako maeneo ya ndani na nje ya uzio wa viwanja vya Mwalimu Nyerere vya maonesho ya wakulima Nanenane Manispaa ya Morogoro ambapo sherehe za sikukuu hiyo zilikuwa zikiendelea na kufanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 39 wa makosa ya uporaji, unyang’anyi wa kutumia nguvu, wizi kutoka maungoni na kujeruhi.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro liliwakuta Watuhumiwa hao
wakiwa na pikipiki moja aina ya SANLG rangi nyeusi yenye namba MC 225 BQT, mapanga 04 na visu 4 ambavyo walikuwa wakitumia kuwapora wananchi waliokuwa wakiingia na kutoka kwenye viwanja hivyo.
Watuhumiwa watafikishwa Mahakamani mara baada ya upelelezi wa awali kukamilika,
Hata ivyo Mnamo tarehe 12/08/2020 majira ya saa 6 usiku huko katika kijiji cha Mbamba wilaya ya Kilosa mkoani Mororgoro mtu mmja anaefahamika kwa jina la SHINJE S/O JILANGILA miaka 30 mkulima mkazi wa Mbamba alimkatakata kichwani shemeji yake aitwae DOTTO S/O NGEME LUHENDE miaka 28 mkulima mkazi wa Mbamba akitumia kitu chenye ncha kali na kumsababishia kifo hapo hapo. Chanzo cha tukio hili ni kwamba.
Mtuhumiwa alimfuata mkewe KURWA D/O NGEME LUHENDE nyumbani kwa shemeji zake kwaajili ya usuluhishio baada ya kuhitilafiana. Ndipo akapewa hifadhi hapo alale ili asubuhi kikao cha usuluhisho kifanyike, Ilipofika majira ya saa 6 usiku alifanya mauaji kwa kaka wa mke wake aliekuwa akimtuhumu kuwa ndio chanzo cha mgogoro wao na bahada ya kutekeleza mauaji hayo mtuhumiwa alikimbia, lakini kutokana na juhudi kubwa za wananchi wakishirikiana na jeshi la polisi walifanikiwa kumkamata akiwa mafichoni. Mtuhumiwa huyo anahojiwa na mara upelelzi wa awali utakapokamilika atafikishwa mahakamani
WITO; Natoa wito kwawananchi wote hasa vijana kuachana na vitendo vya Utaperi, wizi, uporaji, unyang’anyi na kusafirisha dawa za kulevya kwani jeshi la Polisi limejipanga vizuri kuhakikisha uhalifu wa aina hii na uhalifu mwingine unakomeshwa, pia niwaombe wananchi kuendelea kutoa ushirikiano mzuri kwa jeshi la Polisi kwa kufichua uhalifu na wahalifu.
Imetolewana :
Wilbroad William Mutafungwa – SACP
KamandawaPolisi
MkoawaMorogoro
13/08/2020.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment