GGML yaanzisha Bustani ya kuvutia Mjini Geita | Tarimo Blog

 


NA MWANDISHI WETU

Wakazi wa mji wa Geita wanafurahia kuwa sehemu ya mradi wa bustani ya kupumzikia inayofadhiliwa na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) kwa kushirikiana na Halmashauri ya Mji Geita. 

Mradi huo uliotengewa bajeti ya Shilingi milioni 70 kutoka fedha za mfuko wa GGML za uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) zinatarajiwa kukamilisha mradi huo kabla ya mwisho wa mwaka huu.

Akizungumza katika hafla ya kuzindua ujenzi wa bustani hiyo katika kata ya Kalangalala mjini Geita, Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel alisema GGML kwa kushirikiana na Halmashauri ya Geita Mji inatekeleza mradi huo kupitia fedha za Wajibu wa Kampuni kwa Jamii (CSR) kutoka GGML.

Alisema mradi huo unaotekelezwa katika eneo la mita za mraba 4000 katika kata ya Kalangalala mjini Geita, una lengo la kuwapatia wakazi wa Mji wa Geita fursa ya kuwa na eneo la kufanya shughuli mbalimbali zikiwemo kupumzika, kupunga upepo pamoja na kuepuka kero za joto.

“Lengo letu ni kuona wakazi wa Mji wa Geita wanafika katika eneo hili kufurahia upepo asilia sanjari na kuona mnara maalum wenye kumbukumbu ya Mkoa wa Geita.

“Bustani hii itakuwa kivutio pia kwa vile inajengwa kwa tofali za kuvutia kwenye maeneo yote ya kupitia na sehemu za watu kuketi hali ambayo itashawishi watu wengi zaidi kukaa na kujionea uzuri wa Mji wetu wa Geita,”alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Richard Jordinson alisema kuwa Kampuni ya GGML imekuwa ikifanya jitihada kubwa kubadilisha muonekano wa jamii ya Mkoa wa Geita kwa kuanzisha miradi endelevu. 

“GGML tunajivunia kuwa, wakati tunasherehekea miaka 20 ya uwekezaji wetu ndani ya Mkoa wa Geita mwaka huu, tumefanikiwa kutekeleza miradi mingi yenye tija na matokeo chanya ikiwemo mnara wa makutano ya barabara Mjini Geita, masoko, taa za barabarani, vituo vya afya, shule na barabara za lami,” alisema Richard Jordinson.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akimuonyesha mchoro wa bustani ya kisasa Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Richard Jordinson mwingine ni Meneja Mahusiano wa GGML, Joseph Mangilima.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert, Mkurugenzi mtendaji wa GGML Richard Jordinson na Meneja Mahusiano wa GGML, Joseph Mangilima wakiteta jambo baada ya uzinduzi wa ujenzi wa Bustani ya kisasa katikati ya mji wa Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel (mwenye sururu) akichimba msingi katika uzinduzi wa ujenzi wa bustani ya kisasa katikati ya mji wa Geita inayotarajiwa kutumia sh. milioni 70 kutoka GGML.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2