Kampuni mama ya SBL yatangaza mpango endelevu wa miaka 10 | Tarimo Blog

 Na Mwandishi Wetu

 Diageo, kampuni ya kimataifa inayoimiliki Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) imetangaza  mpango madhubuti wa miaka 10 unaolenga kutoa mchango chanya kwa maendeleo duniani kufikia mwaka 2030 ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Umoja wa Mataifa kupitia mpango wake wa Malengo ya Maendeleo endelevu (SDG).

 Kupitia mpango huo wa miaka 10, Diageo itajikita katika sehemu kuu tatu ambazo zimechaguliwa kwa kuzingatia Mpango wa Maendeleo endelevu wa Umoja wa Mataifa. Sehemu hizo ni Kuhamasisha unywaji wa kistarabu, Kuhakikisha ushirikishwa wa jamii katika shughuli mbali mbali, pamoja na kuhamasisha kilimo endelevu.

 Kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita kampuni ya SBL inayomilikiwa na Diageo, imekuwa ikiendesha kampeni ya kuhamaisha unywaji wa kistarabu kupitia kampeni ya ya kitaifa y “Usinywe na kuendesha chombo cha moto” ikishirikiana na wadau mbali mbali kama jeshi la Polisi kitengo cha Usaalama barabarani. Kampeni hii imeweza kuwafikia zaidi ya watu 100,000 wakiwemo madereva bodaboda, madereva wa mabasi na umma kwa ujumla.

 Katika kilimo endelevu, SBL inafanya kazi na mtandao wa wakulima 400 wanaolima mazao kama mahindi, mtama, na shayiri ambao kwa sasa wanasaidia kuipatia kampuni asilimia 80 ya malighafi inayohitaji katika uzalishaji wa bia zake kwa mwaka. Kupitia programu yake ya Kilimo Viwanda, SBL inatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa kilimo ikilenga kusaidia kuongeza wataalamu wa killimo hapa nchini ambao ni nguzo muhimu katika maendeleo ya sekta hii mama

Kwenye ushirikishi wa jamii, SBL imeweza kuchimba visima 17 katika maeneo mbali mbali yenye changamoto ya upatikanaji wa  maji na hivyo kuwezesha jamii na haswa akina mama na Watoto wa kike ambao hubeba mzigo wa kutafuta maji kunufaika na huduma ya maji safi na salama karibu na maeneo yao.

 Akizungumzia kuhusu mpango huo, Afisa Mtendaji mkuu wa Diageo Ivan Menezes alisema, “Tukiwa kama wadau wa biashara duniani, tunao wajibu wa kulinda duniani yetu na kuifanya kuwa sehemu salama ya kuishi kwetu na vizazi vijavyo. Ninayofuraha kubwa kwa mchango wa maendeleo ambao Diageo imeweza kuutoa kufikia leo. Mpango huu mpya utatuwezesha kuendelea kutoa mchango mkubwa Zaidi kufikia 2030.

Kupitia Programu ya Kilimo Viwanda, Kampuni ya Bia ya Sarengeti imekuwa ikitoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wanaosomea kilimo hapa nchini ili kuongeza wataalamu katika sekta mama kwa uchumi wa nchi.

Kampuni ya Bia ya Serengeti kupitia kampeni yake ya maji ni uhai, imekuwa ikichimba visima vinavyowezesha jamii zinazoishi sehemu zenye uhaba wa huduma ya maji kupata huduma ya maji safi na salama.

Madereva boda boba ni moja kati ya kumbi ambalo limekuwa likifaidika na Kampeni ya Usinywe na Kuendesha Chombo cha Moto inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.

Kampuni ya Bia ya Serengeti inafanya kazi na wadau mbali mbali ikiwamo Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani katika kupambana na ajali za barabarani kupitia kampeni yake ya Usinywe na kuendesha chombo cha moto

 


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2