Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
TAASISI ya kuzuia na kupambana na rushwa ,mkoani Pwani imebaini wajumbe wengi wa mabaraza ya ardhi mkoni hapo,wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa katika utendaji kazi wao hali inayosababisha kero kwa wananchi .
Kamanda wa taasisi hiyo mkoani Pwani,Suzan Raymond amesema, katika eneo la uzuiaji rushwa wamefanya uchambuzi wa mifumo miwili katika maeneo ya utoaji haki kwenye mabaraza ya ardhi ambapo ikabaini wajumbe wa mabaraza ya ardhi kuwa vinara wa kulalamikiwa.
Alieleza, haiwezekani kuona eneo kama hilo linakwamisha juhudi za kutoa haki kwa wananchi linakuwa kero kukwamisha utoaji huduma.
Suzan alieleza ,waliobainika kuhusika na matukio ya kuomba rushwa ili kutoa haki wakati ni wajibu wao kuhudumia wananchi wamefunguliwa kesi na kuchukuliwa hatua kulingana na sheria.
Pamoja na hilo ,wamefanya uchambuzi wa mfumo wa utoaji wa vibali vya ujenzi kwa halmashauri zote na kugundua baadhi ya wajenzi wanajenga bila kufuata taratibu za kupata kibali huku wakazi wengi hawafuati utaratibu wa kuomba vibali vya ujenzi kabla ya kujenga na kujikuta wakijenga kiholela na kutokana na utaratibu huo kuwa na urasimu na mianya ya rushwa.
Kamanda huyo anaomba halmashauri mkoani humo ,kuweka mkazo kwenye eneo hilo la vibali kama chanzo cha mapato na kuacha kuchukua muda mrefu kutoa vibali inakuwa vikwazo na kusababisha jamii kutumia njia za mkato kwa kutoa rushwa.
Aidha Suzan ,alibainisha kuwa, katika kipindi cha robo ya mwaka wamepokea malalamiko 136 kati ya hayo malalamiko 79 uchunguzi unaendelea katika hatua mbalimbali."Malalamiko 57 yalionekana kuangukia katika sheria hivyo walalamikaji tuliwashauri na kuelekezwa sehemu husika kwa lengo la kutatua kero zao"
"Kesi 17 ziliendelea kuendeshwa katika mahakama mbalimbali za mkoa ambapo kati ya kesi hizo mpya tatu zilifunguliwa.
Suzan aliwaasa wananchi ,kushirikiana na TAKUKURU kutoa taarifa za washukiwa wa kutoa rushwa au kuomba rushwa na kutumia utaratibu wa PCCB Mobile (TAKUKURU INAYOTEMBEA) kwani wametenga siku moja kila mwezi kila ofisi ya TAKUKURU mkoa,wilaya kufuata wananchi kwa lengo la kusikiliza malalamiko yatokanayo na rushwa.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment