CHONGOLO ATEMA CHECHE RUKWA, ATAKA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO UZINGATIE THAMANI YA FEDHA | Tarimo Blog



KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM,) Daniel Chongolo amemwagiza mkuu wa mkoa wa Rukwa, Joseph Mkirikiti kuunda kikosi kazi cha kukagua na kufanya tathmini ya miradi inayotekelezwa mkoani humo ili kujua ikiwa utekelezaji wake unakidhi thamani ya fedha zilizotumika.

Pia  amesema  hakuridhishwa na miradi walioitembelea hasa katika  sekta ya afya ambayo  inayokabiliwa na changamoto kubwa ya dawa, wataalam, huduma duni kwa wazee pamoja na  maeneo mengine kuwa na  utekelezaji wa miradi isiyoendana na thamani ya fedha iliyotumika.

Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu wa chama hicho,Daniel Chongolo katika kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku mbili mkoani humo aliyoambatana na wajumbe wa Sekretarieti ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa kilichofanyika ukumbi wa mikutano manispaa ya Sumbawanga.

"Naagiza na kukuelekeza  mkuu wa mkoa  uunde timu ya wataalam kwa ajili ya kukagua na kufanya tathmini ya miradi yote inayotekelezwa mkoani kwako ili kujua hali halisi ya kinachoendelea hususani kwenye eneo la thamani ya fedha zilizotumika hapa mambo hayaendi vizuri kabisa" Alisema  Chongolo. 

Alisema  kuwa CCM haiko tayari kuwalea viongozi na watendaji wazembe wanaoonekana kushindwa kutatua kero za wananchi na kuimarisha ustawi wao hivyo kati siku 14 atahitaji kupata ripoti ya utekelezaji wa maelekezo hayo na hatua kali zichukuliwe itakapobainika kuna ubadhirifu ama uzembe ambao unakwambisha ufanisi wa miradi hiyo.

"Nahimiza watendaji wa serikali kuwa waadilifu kwa kuheshimu fedha za umma. Hakikisheni fedha zinazoletwa au kutengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo zinatafsirika kwa wananchi kwa kuwaletea unafuu na kuimarisha huduma za kijamii na kiuchumi kwao." Alisema Chongolo.

Hata hivyo Chongolo alisema atakaporejea Dodoma watawaita mawaziri wanaohusika na sekta za afya maji, aridhi na tamisemi ili kujiridhisha juu ya mipango yao na kujua mkwamo ama urasimu unatokea katika eneo gani na kupelekea huduma kusuasua na kuwa sio za kiwango na ufanisi kwa wananchi.

“Tunataka watueleze nani anasababisha mkwamo katika upatikanaji wa huduma nasema hivi nikitambua  sisi viongozi tunawajibu wa kufuatilia na kusimamia, tutakuwa wakali, ni lazima tuogope fedha ya umma, ukizitumia vizuri zitakujengea heshima, ukizitumia vibaya zitakuvunjia heshima kwa wananchi, hivyo kila mmoja anapaswa kuwa mwadilifu katika  kusimama dhamana aliyopewa,”  Alisema Chongolo.

Alisema kwamba, kila kiongozi na mtendaji katika chama na serikali anawajibu wa kutimiza wajibu wake kwa kuhakikisha upatikanaji wa tija huduma za kijamii unakuwepo kama anavyosisitiza Rais Samia wakati wote.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2