Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. George Simbachawene katika Mkutano wa 23 wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa,Ulinzi na Usalama. Nyuma ya Mawaziri hao aliyevaa barakoa nyeupe ni Katibu mkuu Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine. Mkutano huo umefanyika kwa njia ya video leo Jumatano 07.07.2021 Jijini Dar es Salaam.
***************************
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeeleza nia yake ya kuwa na wajumbe katika Majukwaa ya wazee na usuluhishi wa migogoro katika Kamati ya Asasi ya Siasa,Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameeleza nia hiyo ya Tanzania katika mkutano wa 23 wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa,Ulinzi na Usalama uliofanyika kwa njia ya Mtandao Jijini Dar es Salaam.
Balozi Mulamula ameongeza kuwa Jukwaa la Wazee na Jukwaa la Usuluhishi wa migogoro huundwa na watu mashuhuri wakiwemo Wakuu wa Nchi na serikali wastaafu ambao wana utaalamu wa masuala ya usuluhishi wa migogoro katika nchi wanachama.
Kuhusu suala la viza ya pamoja inayoruhusu wananchi wa nchi wanachama kuruhusiwa kutembelea nchi nyingine bila viza Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. George Simbachawene amesema Tanzania inaendelea vizuri na suala hilo ispokuwa kwa baadhi ya Nchi ambazo bado zipo katika mazungumzo ya kufikia makubaliano hayo
Mkutano huo wa 23 wa Kamati ya Mawaziri wa Asasi ya Siasa,Ulinzi na Usalama umetanguliwa na kikao cha ngazi ya Maafisa Waandamizi ambapo ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Joseph Sokoine.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment