Ludewa:Ashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji | Tarimo Blog


Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mtu mmoja anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Njombe kwa tuhuma za kufanya mauaji ya mtu mwenye umri wa miaka 34 (majina yamehifadhiwa kwa ajili ya upelelezi) mkazi wa kijiji cha Njelela kata ya Mundindi wilayani Ludewa mkoani Njombe na kuahidiwa kulipwa laki moja.

"Kwa kweli amefanya mauaji katika Hali isiyokua ya kawaida yeye aliahidiwa kupewa shilingi laki moja na alipewa hela za kutanguliza shilingi 40,000 na kwenda kutekeleza mauaji hayo"alisema Kamanda Issah.

Kamanda wa polisi mkoa wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema polisi walikwenda kuangalia tukio na kukuta mtu amefariki na marehemu alikua na Pikipiki yake baada ya kuuwawa,muuaji kachukua Pikipiki ya marehemu na kutembea nayo mjini.

"Muuaji alichukua pikipiki ya marehemu na kutembea tembea nayo mjini na kukamatwa nayo alipoulizwa yeye alidai amepewa kazi ya kuua huyu na kupewa shilingi 40,000 bado shilingi 60,000 na kweli tuliweza kumtafuta mtu aliyetoa hela hiyo naye tumemkamata hayo ni mafanikio"kamanda amesema.

Kamanda Issah ametoa wito kwa jamii kuacha kupokea fedha ili kufanya uhalifu wa kuua au kumsababishia mtu apate matatizo ya aina yoyote ile sambamba na kuacha kukodiwa kwa jambo lolote baya.

"Eti tunamuoji kwanini mmemuua anasema walikua wanagombea mashamba na kama mnagombea mashamba sheria zipo.Tunashauri wanaNjombe fateni sheria acheni kujichukulia sheria mikononi kitu ambacho ni tatizo kubwa ambalo linaweza likaleta madhara katika jamii nzima"amesema Kamanda Issah.

Wakati huo huo jeshi la shi la polisi mko wa Njombe limesema limejipanga kuhakikisha usalama wa maeneo yake kipindi cha sikukuu za krismas na mwaka mpya.

"Tumejipanga vizuri kuanzia sehemu za ibada,makazi ya watu mpaka maeneo ambayo watu wanasheherekea na kutokana na Hali kama hiyo,tumejipanga pia kufanya doria za miguu,magari,pikipiki na doria ficha ambazo zitakua zinaangalia maeneo yenye uhalifu ambao ni sugu"amesema.

Pia amesema jeshi la polisi litashirikiana na vyombo vyengine vya ulinzi na usalama katika kuhakikisha usalama wa Njombe unakuwepo na unaendelea kuwa na utulivu kwa muda wote wa sherehe ambazo zinaendelea.

Kamanda amewataka wananchi kuepuka misongamano ambayo haina ulazima ili kuepuka ugonjwa wa Uviko 19.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2