Na Bakari Madjeshi, Michuzi TV
TAKWIMU zinaonyesha uandikishaji Watoto katika Shule za awali, mkoa wa Manyara umefanikiwa kuongoza kwa zaidi ya asilimia 50 (57.99%) ya uandikishaji wa Watoto hao katika mikoa 5 huku mkoa wa Katavi ukiburuza mkia kwa zaidi ya asilimia 8 (8.39%) katika mikoa 5 kwenye takwimu hizo.
Takwimu za uandikishaji Watoto kwa Shule za awali jumla ya Wanafunzi 1, 363, 834 wanatarajiwa kuandikishwa mwaka huu wa masomo, wakiwemo Wanafunzi wenye mahitaji maalum 6,376.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Ummy Mwalimu amesema kuwa takwimu za matokeo ya uandikishaji wa Wanafunzi wa Darasa la Kwanza zinaonyesha jumla ya wanafuzu 1,581, 823 (Wavulana 788,620 na Wasichana 793,203) wanatarajia kuandikishwa.
Mhe. Ummy amesema idadi hiyo inalinganishwa mwaka 2021 ambapo Wanafunzi 1,549,279 wakiwemo Wavulana 775,339 na Wasichana 773,940 wakiwemo Wanafunzi wenye mahitaji maalum 10,645 wanatarajiwa kuandikishwa sawa na Wavulana 5,724 na Wasichana 4,921.
Mhe. Ummy amesema kuwa uandikishaji wa Wanafunzi hao ulianza Novemba 2021 na unaendelea ambapo hadi kufikia Desemba 2021 jumla ya Wanafunzi 663,486 wakiwemo Wavulana 329,538 na Wasichana 329,538 wakiwa tayari wameandikishwa ambayo ni sawa na asilimia 41.94% ya Wanafunzi waliondikishwa katika Shule za Serikali.
Hata hivyo, amesema mkoa wa Manyara umeendelea kuongoza kwa zaidi ya asilimia 70 (70.95%) Njombe (62.06%) Singida (54.23%) Dodoma (54.23%) Lindi (52.46%). Wakati mikoa mingine takwimu zake ziko chini katika uandikishaji huo ni Rukwa (18.62%) Katavi (18.83%) Shinyanga (26%) Mwanza (26.26%) na Mtwara (27.98%).
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment