Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde akiwa ameongozana na Diwani wa Kata ya Mkonze Mh. David Bochela wamefanya ukaguzi wa ujenzi wa daraja kubwa la kivuko katika Mtaa wa Nzinje,Jijini Dodoma.
Daraja hilo ambalo linajengwa chini ya TARURA litakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Mtaa wa Nzinje na maeneo jirani ambao kipindi cha mvua wamekuwa wakipata mkwamo mkubwa wa kuvuka na kuunganishwa na maeneo mengine kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.
Akishukuru kwa niaba,Mbunge Mavunde ameishukuru serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuitengea TARURA fedha za kutosha kugharamia ujenzi wa barabara,mitaro na madaraja Jijini Dodoma hali itakayopelekea maeneo mengi kupitika kwa urahisi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment