RC Rubirya akabidhiwa madarasa 43 Ludewa yaliyokamilika 100% | Tarimo Blog

Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya amepokea na kuzindua madarasa 43 yaliyokamilika 100% kwa shule 16 za halmashauri ya wilaya ya Ludewa na madarasa 4 yaliyokamilika 50% kwa shule ya sekondari Makonde yanayojengwa kupitia Mradi No.5441-TCRP (Fedha za Uviko-19) na kuagiza kukamilishwa mapema madarasa yaliyobakia.

Akizungumza kabla ya kukabidhi mradi wa madarasa 43 yaliyokamilika kwa 100% mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bwana Sunday Deogratius amesema, halmashauri ya wilaya ya Ludewa kiasi cha mil 940 zitokanazo UVIKO-19 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 47 vya madarasa na samani zake lakini hadi sasa madarasa 4 yanayojengwa katika shule ya sekondari Makonde yanaendelea na ukamilishwaji.

“Ujenzi umekamilika kwa 100% kwa shule 16 na 50% kwa shule ya Sekondari Makonde.Changamoto kubwa kwa shule ya sekondari Makonde ni hali ya jeografia ya eneo pamoja na mwamko mdogo wa wananchi kujitolea katika shughuli za kijamii”Sunday Deogratius mkurugenzi Ludewa akikabidhi madarasa kwa RC Njombe

Ameongeza kuwa “Kwa niaba ya wananchi wa Ludewa ninatoa shukrani kwa Rais wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kufanikisha utekelezaji wa mradi huu.Ninaahidi kusimamia kwa karibu ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa shule ya sekondari Makonde ili vikamilike kabla ya tarehe 15 Januari 2022” Sunday Deogratius mkurugenzi Ludewa akikabidhi madarasa kwa RC Njombe

Kwa upande wake mkuu wa wilaya hiyo Mh.Adrea Tsere amesema wataendelea kuongeza nguvu ili kukamilisha madarasa hayo yaliyojengwa kwa aina moja.

“Madarasa hayo yote 43 hata viti na meza magari yapo site kusambaza na madarasa tumeyajenga kwa aina moja”alisema Adrea Tsere

Mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya amepongeza na kuridhishwa kwa ubora ulioonekana katika madarasa yaliyokamilika.

“Nimeridhika sana na ubora wa kazi uliofanyika hapa na mmeweza kuweka sakafu ya vigae katika vyumba vya madarasa yote ni ubunifu mkubwa uliofanyika hapa”alisema Rubirya
Mkuu wa mkoa wa Njombe akikata utepe kuonyesha uzinduzi wa madarasa 43 yaliyokamilika kwa wilaya ya Ludewa.

Mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya akifurahi ubora wa meza na viti vilivyotengenezwa wilayani Ludewa



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2