*Mkuu wa Chuo Makasanga aahidi neema za kozi bobevu kuanzishwa.
Na Chalila Kubuda,Michuzi TV
WAHITIMU wa Chuo cha Tehema VETA Kipawa wameaswa kuwa wao ndio tegemeo katika mafunzo ya Tehama kwani serikali iko kwenye mpango wa matumizi ya tehama katika mpango wa tatu.
Teknolojia ya Tehama inabadilika kila siku hivyo wahitimu ni lazima kuongeza maarifa ya ubunifu kuhakikisha hakuna mtu wa kuachwa nyuma.
Ameyasema hayo Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Dar es Salaam Angelius Ngonyani wakati wa Mahafali ya 10 ya Chuo cha Tehama VETA Kipawa yaliyofanyika Desemba 31 katika viwanja vya Chuo hicho.
Amesema wapo watu ambao kuwa Chuo cha Tehama VETA kipawa kwa kozi zake zinaendana na wakati juu ya matumizi ya Tehama hivyo wahitimu wana kazi ya kuonyesha ubunifu wa kuleta chachu katika sekta ya Tehama.
Ngonyani amesema kuwa changamoto ya ajira isiwe kikwazo cha kufanya mhitimu kulala bali ni kuonyesha njia ya kujiajiri na kutoa faraja kwa wazazi na kuleta matokeo chanya kwa taifa kuwa na nguvu kazi yenye uzalishaji.
Amesema kuwa kuhutimu sio kukaa na vyeti bali kuonyesha tofauti kwa kuwa na ubunifu na weledi katika kufanya kazi ndio hapo nafasi cheti au shahada ya kwanza,hadi ile ya Profesa inaonekana.
Ngonyani amesema ujuzi ukitumika katika ubunifu utasaidia kutatua changamoto nyingi zilizopo katika jamii ambapo wataalam ndi nafasi yao ya kutatua.
Mkuu wa Chuo cha Tehama VETA Kipawa Mhandisi Sospeter Mkasanga amesema Chuo hicho tangu kilipoanza mwaka 2010 hadi 2021 zaidi ya wanafunzi 9000 wameweza kuhitimu na idadi kwa idadi ya kila mwaka kuongezeka.
Mhandisi Mkasanga amesema kuwa Chuo cha Tehama VETA Kipawa ndicho chuo pekee cha kinachotoa mafunzo ya Tehama hivyo ni jambo ambalo kwa Teknolojia inavyokuwa mahitaji yanaongezeka kwa ajili ya kwenda kutatua changamoto za Tehema kwa wananchi.
Mkasanga amesema kuwa kuna kozi zitaanzishwa za ubobevu ikiwemo ya tehama nia kufanya wahitimu kuwa na myumbuliko wa kufanya kazi kwa viwango vya juu.
Aidha Amesema tangu walipoanza Chuo hicho wahitimu wamekuwa wakiajirika sehemu mbalimbali na wale wanaojiajiri nao wamekuwa na mafanikio.
Amesema kuwa mafunzo ya ujuzi duniani kote ni mafunzo muhimu kwa kuwa wahitimu wa kozi za ufundi ni watendaji wazuri kwenye sehemu hasa za uzalishaji na wanatagemewa na serikali imedhamiria kuwa na wawekezaji katika sekta ya viwanda ambapo asilimia kubwa tehema inahusika.
Aidha amesema jamii ikitambua nafasi ya mafundi na kuwalipia ada watoto wao kusomea ufundi wa aina mbalimbali itasaidia kupunguza tatizo la ajira.
Alisema kuwa wahitimu kutoka VETA wamekuwa wakiajiliwa katika viwanda mbalimbali huki wengine wakishika wadhifa wa kuongoza vitengo.
”Kwa sasa kuna Tanzania ya viwanda hakika unataka uwepo wa wataalamu wengi kwenye viwanda na wenye ujuzi mbalimbali." Amesema.
Amesema kuwa pia kumekuwa na changamoto ya idadi ndogo ya wanawake kusomea masomo ya ufundi ambapo amebainisha kuwa wanawake wengi wamekuwa na dhana ya kuwa masomo hayo ni ya wanaume tu.
Mhandisi Mkasanga amesema wapo wanawake ambao wamekuwa wakifanya vema kwenye masomo mbalimbali chuoni hapo na kuwa chuo kimeweka mfumo mzuri wa kuwawezesha wanawake kusoma kwa ufanisi hivyo wameomba wazazi wawapeleke katika chuo hicho.
Amesema ”Wanawake masomo ya ufundi pia yanawafaa tena sana kwa kuwa wanaweza kufanya karibia kila kazi ya ufundi na wapo ambao wamehitimu hapa na wamekuwa wafanyakazi wakubwa na wazuri tu huko walipo.”
Kwa upande Mwakilishi wa Wazazi Dominata Marwa amesema wahitimu waonyeshe uadilifi katika kazi na kuacha wizi kwani inaleta sifa mbaya kwa waajiri na hata wawekezaji wa nje ambao mwisho siku wanaleta wafanyakazi kutoka nchini kwao.
Amesema kuwa wahitimu wakipata kazi watangulize uzalendo kwa kujituma kwa kuamini ajira hizo zinawategemezi wengi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment