SAFARI YA KUENDELEA KUOMBA KURA KWA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM YASHIKA KASI | Tarimo Blog

Ad

Ads1
*Dk.Magufuli ashauri watanzania kuwa makini katika kuchagua viongozi


Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Busega 

SAFARI ya mgombea urais kwa tiketi ua Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dk.John Magufuli imeendelea tena leo akiwa njiani akitokea mkoani Mara kwenda Mkoa wa Mwanza ambapo msafara ulikuwa ukisimamishwa mara kwa mara na maelefu ya Watanzania waliokuwa kando ya barabara.

Akiwa katika mikutano hiyo ya kampeni Dk.Magufuli amewaomba Watanzania kuwa makini katika kuchagua viongozi katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 mwaka huu na kwamba ni bora kukosea kuoa mke au mume kuliko kiongozi kwani madhara yake yatakuwa kwa kipindi cha miaka mitano.

Hivyo katika uchaguzi huo ,mgombea huyo ambaye ni kipenzi cha maelfu ya wananchi amewaambia ni vema wakamchagua yeye kwa nafasi ya urais pamoja na wabunge na madiwani kutoka CCM.

"Nawaomba wananchi kuhakikisheni hamchanganyi kitunguu na gongo kwa kuchagua viongozi wa vyama tofauti tofauti katika eneo moja kwani kwa kufanya hivyo mtanipa shida katika kushughulikia kero za wananchi.CCM ndio tunajua changamoto za watanzania,ndio maana tumekuja kwenu kuomba ridhaa ya kuongoza kwa mitano mingine,"amesema na kusisitiza

"Nawaambia ukweli bora mtu ukosee kutafuta mume au mke lakini sio kukosea kuchagua kiongozi.Chagueni wabunge na madiwani wa CCM ili fedha za maendeleo zinapokuja na wakishindwa kutekeleza yaliyokusudiwa nitawabana , mkileta tofauti sitaweza lakini wa CCM nitamshughulikia,"amesema.

Amefafanua katika uchaguzi hawachagui sura ya mtu kwani hata sura yake ni mbaya wanachagua vyama,"amesema na kuongeza ni vema Watanzania wakahakikisha wanaichagua CCM na wakifanya makosa watajuta huku akisisitiza yeye huwa hafichi anasema ukweli.

Ametoa mfano ukienda Bunda hakuna taa za barabarani kwasababu aliwaambia lakini hawakusikia wakachagua upinzani.Maendeleo lazima yapelekwe mahali ambapo mtu anapata ushirikiano."Kazi kwenu kuamua hamtachagua CCM majuto yatabaki kuwa mjukuu."

Hata hivyo akihutubia maelfu ya wananchi waliokuwepo kwenye mikutano hiyo na amezungumzia watu ambao wamekuwa wakidai ndege ambazo zimenunuliwa hazisaidii ambapo amewajibu "Wanaosema ndege hazisaidii kwani dawa na vifaa tiba zinakuja kwa baiskeli?"

Ameendelea kuhoji hivi nchini kwetu kuna viwanda vya  X-ray."Tukitumia ndege zetu maana yake hata gharama zinakuwa na unafuu.Hivi wataliii wanapokuja nchini wajakuja na bodaboda?"

Akiwa eneo la Nyamikoma wilayani Busega Dk.Magufuli amefafanua aliahiadi kujenga kwamba baada ya uchaguzi mkuu kumalizika atahakikisha anajenga shule nyingine katika eneo hilo.

Hata hivyo amesema maendeleo ambayo yamefanyika katika hilo yanadhihirisha namna ambavyo katika kipindi cha miaka mitano Serikali imefanya mambo makubwa ya maendeleo.

Amewaomba wananchi wa Busega kuichagua CCM  kwani Ilani ya Uchaguzi Mkuu imepanga mikakati mingi ya kufanya kwani hata  barabara inayopita hapo imeanza kuharibika, lazima katika kipindi cha miaka mitano itengenezwe kwa kiwango cha lami huku akielezea miradi ya maendeleo iliyotekelezwa na kuleta maendeleo.

Hata hivyo baada ya kutoka Busega aliendelea na safari ya kwenda Jijini Mwanza aliendelea kuelezea hatua kwa hatua maendeleo ambayo yamepatikana,hivyo anaomba miaka mitano mingine amalizie kazi aliyoianza.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

Sponsor Ad

Ads2

Post a Comment

Previous Post Next Post