Charles James, Michuzi TV
AGIZO la Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Dk Dorothy Gwajima la kulitaka Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi wake limetekelezwa na baraza hilo kuwapata viongozi wake.
Baraza hilo limekutana jijini Dodoma na kufanya uchaguzi wake ambalo sasa litaundwa na viongozi waliochaguliwa ambapo Mwenyekiti mpya ni Lilian Badi ambaye ameahidi kuyatekeleza yale yote ambayo ameahidi wakati wa kuomba kura.
Badi ametangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huo na Mwenyekiti wa Kamati ya mpito, Flaviana Charles iliyosimamia uchaguzi wa kuwapata viongozi hao.
Flaviana alimtangaza Badi kuwa mshindi baada ya kupata kura 21 akifuatiwa na aliyekua akigombea nae, Jane Magigita ambaye amepata kura nane.
Nafasi nyingine ambayo iligombewa ni ya Katibu Mkuu ambapo wajumbe walimchagua Revocatus Sono kwa kura 22 akifuatiwa na Gift Kilasi ambaye alipata kura Saba.
Nafasi nyingine iliyogombewa ni ya mweka hazina ambapo wajumbe wamemchagua John Kiteve kwa kura 15 akimpiku Miraji Malinda aliyepata kura 13 wakati Gaidon Haule akipigiwa kura za ndio na wajumbe wote katika nafasi ya Kamati ya Fedha na Utawala.
Pia katika kamati ya maadili wajumbe hao wamemchagua Novatus Marandu ambaye amepata kura 15 na Kamati ya Maendeleo na Uwezo akichaguliwa Rhobi Samweli, Kamati ya Utandaa na Mawasiliamo akichaguliwa Asifiwe Mallya huku wajumbe wanne wa Bodi wakiwa ni Jane Magigita,Revocatus Sono,Paulina Majogoro na Baltazari Komba.
Mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Lilian Badi ameomba ushirikiano kwa wajumbe wa baraza hilo huku akiahidi kutekeleza yale ambayo aliahidi wakati wa kuomba kura.
“ Tumezungumza mengi na tumetoa ahadi nyingi kwa pamoja tukishirikiana tutaenda kuyafanyia kazi yale tuliyoaahidi kikubwa naomba ushirikiano,”amesema.
Kwa upande wake,Katibu mpya wa Baraza hilo,Sono amewashukuru wote waliomwamini kwa kumpigia kura ambapo amedai kwamba mchakato huo haukuwa mdogo.
Naye,Mwekahazina mpya Kiteve amesema watakuwa wasiri wa vikao kwa kutokutoa siri huku akidai kwamba watatoa ushauri sahihi kwa viongozi wa juu.
“Tutaendelea kumshauri Mwenyekiti pamoja na wengine tutakupa ushauri unaofaa (Mwenyekiti) sisi hatutoi siri na tutakuwa wasiri wa vikao,’’amesema.
Naye Mbunge wa Viti Maalum kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs) Neema Lugangira amewataka viongozi wapya kutokufanya kazi kwa kificho na badala yake wanatakiwa kuwa wawazi katika mambo yao pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili waweze kuonekana.
Katibu Mkuu mpya wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyo ya kiserikali (NaCoNGO), Revocatus Sono akizungumza mara baada ya kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya wa baraza hilo uliofanyika jijini Dodoma kufuatia AGIZO la Waziri wa Afya Dk Dorothy Gwajima kuwataka wafanye hivyo.
Mweka Hazina mpya wa NaCoNGO, John Kiteve akizungumza mbele ya wajumbe wa baraza hilo baada ya kuchaguliwa katika uchaguzi wa kuwapata viongozi wa baraza hilo uliofanyika jijini Dodoma.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment