Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV
KAMATI ya Uchaguzi wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NaCONGO ) imesema uchaguzi huo unatajia kufanyika Julai 8 mwaka huu na hatua hiyo imekuja baada ya kukamilika kwa chaguzi katika ngazi ya Wilaya, Mikoa na Mashirika.
Akizungumza leo Julai 7,2021 Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi Fraviana Charles amesema Julai 8 mwaka huu uchaguzi utafanyika katika ngazi ya Taifa wa baraza hilo huku akifafanua katika ngazi za wilaya ,mikoa na mashirika uchaguzi umefanyika kwa mafanikio, hivyo kazi kubwa iliyobakia ni kuchagua viongozi ngazi ya kitaifa.
Amesema uchaguzi huo utafanyika ukumbi wa Royal Village Jijini Dodoma na yeye jukumu lake kubwa ni kuratibu na kusimamia uchaguzi wa Baraza la Taifa Mashirika yasiyokuwa ya serikali na tayari maandalizi yote yamekamilika .
Amesema baraza litakaloundwa litakuwa na wawakilishi au wajumbe 30 kati ya hao 26 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na mjumbe mmoja kutoka kila mkoa na wajumbe wanne watachaguliwa kutoka makundi maalum.
Amesema makundi hayo ni mashirika ya kimataifa ,watu wenye ulevmavu na watoto pamoja na Vijana huku akitumia nafasi hiyo kutoa taarifa ya matokeo ya uchaguzi wa baraza la Taifa la mashirika yasiyoyaserikali katika ngazi ya Wilaya uliofanyika Juni 26 mwaka huu.
Fraviana amesema kwa ujumla mchakato wa uchaguzi wa wajumbe wa NaCONGO ngazi ya wilaya ,mikoa na wa makundi maalumu ulifanyika kwa mafanikio, mpaka kufikia hatua ya kupata wajumbe wote wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali."Tunatarajia uchaguzi ngazi ya Taifa utafanyika kwa ueledi na mafanikio makubwa ili kupata viongozi wa baraza jipya kwa maana ya Mwenyekiti ,Katibu Mkuu ,pamoja na Mweka Hazina wa Baraza,"amesema.
Amefafanua baada ya uchaguzi huko kufanyika Julai 8, Julai 9 wataapishwa na Julai 10 viongozi wapya watakabidhiwa nyaraka na ofisi kutoka kwa uongozi uliomaliza muda wake.Kuhusu uchaguzi wa ngazi za wilaya ,mikoa na mashirika Katibu Mtendaji wa Kamati ya Uchaguzi ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa FCs Francis Kiwanga amesema mchakato wa uchaguzi huo uliopita changamoto zilikuwepo lakini wanashukuru wamemaliza salama na sasa wanakwenda kumaliza ngazi hiyo ya Taifa.
Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NaCoNGO ) Wakili Fraviana Charles (kulia) akiwa na katibu Mtendaji wa kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga (kushoto) wakati wa mkutano wao na waandishi wa habari kuelekea Uchaguzi Mkuu huo uliofanyika leo Julai 6,2021 Jijini Dar es Salaam.Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NaCoNGO ) Wakili Fraviana Charles (kushoto) akijadiliana jambo na Meneja Idara ya Mahusiano na Maendeleo wa (FCS) Nasim Losai.
Katibu Mtendaji wa Kamati hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Francis Kiwanga akizungumza na waandishi wa habari (hawamo pichani) juu ya mchakato mzima wa kuwapata viongozi wa Wilaya na Mikoa wa Baraza la Taifa la Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NaCONGO ) na kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Julai 8, 2021.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment