Na Amiri Kilagalila,NJOMBE
Polisi wilaya ya Ludewa mkoani Njombe imekiri kupungua kwa vitendo vya uvutaji bangi,uchezaji wa kamari,wizi,ubakaji,ulevi na uzurulaji kutokana mchezo wa mpira wa miguu kupitia ligi ya wilaya iliyokuwa ikiendelea wilayani humo kwa kudhaminiwa na mbunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa kituo cha polisi Ludewa SP.H.A.Gawile kwa niaba ya OCD wa kituo hicho cha polisi wakati wa ufunguji wa ligi hiyo uliofanyika katika uwanja wa halmashauri ya wilaya ya Ludewa uliopo mtaa wa Kiyombo wilayani humo.
Gawile amesema kiwango cha matukio hayo yamepungua kwa kiasi kikubwa wakati michezo hiyo ikiendelea tangu ilipozinduliwa tarehe 4/12/2021 na kuhitimishwa tarehe 23/12/2021 kutokana na vijana wengi kujikita zaidi kufuatilia michezo.
Licha ya kupungua kwa matukio hayo Gawile amesema michezo ipo katika miradi ya polisi Jamii na husaidia kudumisha amani,upendo na mshikamano katika jamii.
Vile vile amesema vijana wengi wameweza kujitangaza kupitia michezo hiyo na upo wezo mkubwa wa kupata nafasi kupitia vilabu vya ngazi ya juu.
Aidha ametoa wito kwa wachezaji kuweza kushiriki katika ulinzi shirikishi katika maeneo yao ili kusaidia kupunguza zaidi uhalifu.
Hata hivyo ametoa wito kwa jamii wilayani humo kusheherekea sikuku za Krismass na mwaka mpya kwa utulivu mkubwa na amani.
Katika mashindano hayo yaliyomalizika salama wilayani Ludewa timu ya Lake Star kutoka Manda imefanikiwa kuwa mshindi wa kwanza na kupata shilingi laki sita na nusu (650,000),mshindi wa pili ni Ludewa Fc aliyekabidhiwa shilingi laki nne na nusu (450,000) na mshindi wa tatu ni bodaboda Fc aliyepata shingi laki mbili na nusu (250,000
)
)
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment