WAZIRI WA FEDHA ATEMBELEA KIWANDA CHA NGUO CHUMBUNI ZANZIBAR | Tarimo Blog

Ad

Ads1

Na Khadija Khamis –Maelezo

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa amesema kukamilika kwa kiwanda cha nguo, (Basra Textilemilis L.T.D ) kutasaidia kuzalisha ajira mpya kwa vijana wa Zanzibar .

Hayo aliyasema wakati alipofanya ziara ya kutembelea kiwanda hicho ambacho kinaendelea na matayarisho ya kuanza kazi ya kuzalisha vitambaa mbali mbali ikiwemo vitenge, sare za wafanyakazi na wanafunzi , Madira na nyenginezo kilichopo chumbuni .

Alifahamisha kuwa ujenzi wa kiwanda hicho utazidisha ongezeko la ajira kwa vijana ambazo zinatarajiwa kutolewa kwa awamu tofauti jambo hili litasaidia vijana wengi kujipatia fursa hiyo .

“Kazi zenu wenyewe vijana, mjitokeze kufanya kazi katika kiwanda hichi ili kujipatia kipato chenu cha halali,”alisema Balozi Ramia .

Aidha amefahamisha kuwa kutakuwa na utaratibu maalumu wa mpango ambao unatarajiwa kugawiwa katika maeneo matatu kwa awamu tofauti ambapo katika awamu ya kwanza tayari imeshaanza .

Alisema Wizara ya Fedha na Mipango itaendelea kuongeza nguvu kwa wawekezaji ambao wanania ya kuwekeza miradi yao Zanzibar sambamba na kuwapunguzia kodi za mali ghafi ambazo wanaziingiza nchini .

Aidha aliwataka wakaazi wa eneo hilo kumsaidia muekezaji huyo kutunza eneo hilo ili usitokezee uharibifu wa mali na kufanya kazi zake kwa amani

Nae Meneja wa Kiwanda cha Basra textilemills L.T.D Ali Idrissa Mohamed ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa mashirikiano ya pamoja katika kuwaunga mkono kwa lengo la kuendeleza kiwanda hicho .

Aidha amesema zaidi ya dola milioni 23 zimeshatumika hadi sasa kwa shughuli za utayarishaji wa kiwanda cha Basra Textilemills LTD na kutarajia

Vile vile ameeleza kuwa wanatarajia kuajiri vijana kwa awamu tatu kwa idadi tofauti,vijana 453 kwa awamu ya kwanza 1200 awamu ya pili na 1600 kwa awamu ya tatu .

Ziara hiyo ni miongoni mwa ziara ya Mhe Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa alizotembelea maeneo mbali mbali ya vianzio vya kiuchumi . 
 Mkurugenzi  wa Kiwanda cha Nguo cha Basra (Basra Textilemills LTD )  Ahmed Osman Ahmed akimtembeza  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe.Balozi  Mohamed  Ramia Abdiwawa wakati alipofanya ziara katika kiwanda hicho  kilichopo  chumbuni. 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

Sponsor Ad

Ads2

Post a Comment

Previous Post Next Post